Shaffih Dauda: Pendeni Mpira

Shaffih Dauda: Pendeni Mpira

 Ukisikia kimeumana ndiyo hii sasa kutoka ukurasa wa Twitter wa mtangazaji mahiri wa michezo Tanzania, Shaffih Dauda ameamua kutoa ushauri wake kuhusiana na Haji Manara pamoja na wapenzi wa soka.

Hiyo ni baada ya aliyekuwa msemaji wa klabu ya Simba Manara kuamisha majeshi na kuhamia katika kalabu ya Yanga.

“Wale waliompenda Haji, tayari yupo Yanga na wale wanaoipenda Simba basi yenyewe ipo na itaendelea kuwepo, Mjifunze sana kuupenda mpira kisha timu, mkipenda watu watawashangaza sana” ame-tweet Shaffih Dauda.

Aisee tuambie bhana hapo chini, weka comment yako unakubaliana na ushauri wa Shaffih Dauda au wewe unasemaje?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags