Serikali yaomba muda kukamilisha upelelezi kesi ya msanii wa fani ya uigizaji, Joyce Mbaga (32) maarufu Nicole Berry na mwenzake, Rehema Mahanyu (31), wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.
Msanii huyo na mwenzake walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni inayoketi Kinondoni, Jumatatu Machi 10, 2025, wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, kutokana na kupokea amana (fedha) kutoka kwa umma bila kibali cha Benki Kuu (BoT).
Kesi hiyo ilipotajwa leo, mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali Rhoda Kamungu ameieleza Mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika.
“Mheshimiwa Hakimu kesi hii imepangwa leo kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika. Hivyo tunaiomba Mahakama yako itupangie tarehe nyingine ya kutajwa,” amesema Wakili Rhoda.
Taarifa hiyo ya upelelezi kutokukamilika na maombi ya kupangiwa tarehe nyingine ya kutajwa, kwao hiyo inamaanisha Serikali kupewa muda wa kuendelea na upelelezi.

Leave a Reply