Serikali kupeleka muswada bungeni wa mabadiliko ya sheria ya ndoa

Serikali kupeleka muswada bungeni wa mabadiliko ya sheria ya ndoa

Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imesema ina nia ya kupeleka muswada wa mabadiliko ya sheria ya ndoa ya mwaka1971 katika Bunge hili la Bajeti linaloendelea, ili kuweka umri wa miaka 18 kama umri wa chini wa kuolewa na kuoa.

Waziri wa Katiba na Sheria,Dr. Damas Ndumbaro amesema hayo jana ofisi kwake, Mtumba jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na jukwaa la wakurugenzi wanawake waliowakilisha mashirika takribani 400 yanayotetea haki za wanawake, wasichana na watoto nchini Tanzania.

Wakurugenzi hao wamemhakikishia Waziri na ofisi yake kutoa ushurikiano katika kuhakikisha mchakato huo unapelekea kuwa na sheria nzuri yenye malengo ya kijinsia kwa ajili ya kuimarisha ulinzi kwa watoto hasa watoto wa kike.

Ikumbukwe tuu sheria ya ndoa inayotumika sasa ni ya mwaka 1971 (kifungu namba 13), mtoto wa kike anaweza kuolewa kuanzia umri wa miaka14 kwa ridhaa ya mahakama na kifungu namba 17 kinasema anaweza kuolewa kwa miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi lakini sheria hiyohiyo inasema mtoto wa kiume ananza kuoa kuanzia umri wa miaka 18.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags