Serikali kukuza ajira kwa vijana, Sekta ya sanaa na burudani

Serikali kukuza ajira kwa vijana, Sekta ya sanaa na burudani

Serikali imeweka wazi kuwa inampango wa kukuza ajira kwa vijana katika sekta ya michezo, sanaa na burudani.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi Juni 13, 2024 na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba akiwa bungeni, jijini Dodoma, wakati alipokuwa akiwasilisha mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/25, ambapo ameeleza kuwa Serikali inampango wa kupanua ajira kwa vijana katika sekta ya Sanaa na Burudani.

“Serikali ya Awamu ya Sita inatambua umuhimu wa michezo, sanaa na burudani katika kukuza ajira hususani kwa vijana. Kwa kuzingatia hilo, Serikali imeendelea kuwaunganisha wasanii wa Tanzania na soko la kimataifa mbalimbali na kuhakikisha kuwa kazi za ubunifu wao zinalindwa,” amesema

Hata hivyo, serikali imetenga bajeti ya Sh 285.3 bilioni katika sekta ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo kwa Mwaka 2024/25, huku bajeti hiyo ikiipiku ya mwaka 2023/24 ambapo ilitengewa Sh 35.4 bilioni kwa ajili ya kukuza, kuendeleza sanaa, michezo na utamaduni.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags