Sean Paul afunguka kolabo yake na Beyonce ilivyotokea

Sean Paul afunguka kolabo yake na Beyonce ilivyotokea

Mwanamuziki mkongwe kutoka nchini Jamaica, Sean Paul, amefunguka ushirikiano wake na mwimbaji wa pop wa Marekani, Beyoncé ulivyoanzia mpaka ngoma yao ya ‘Baby Boy’ kuweka rekodi kote ulimwenguni.

Paul ameyasema hayo katika mahojiano yake na The  Hollywood Reporter akidai kuwa Beyoncé alikuwa mwanga kwake baada ya kushirikiana kwenye kolabo ya wimbo wake wa ‘Baby Boy’ kutoka kwenye albamu yake ‘Dangerous Love’ iliyotoka mwaka 2003.

Aidha mwanamuziki huyo wa dancehall ambaye anaumri wa miaka 51 amedai kuwa wimbo huo ulifungua njia ya kukubalika kwa dancehall duniani na kuweka historia ya kufanya kazi na Beyoncé.

Hata hivyo Paul amesema kuwa aliwahi kufanya kazi na wasanii kama Busta Rhymes, Clipse, na Blu Cantrell, ambao walikuwa na mwelekeo wa hip-hop zaidi, lakini Beyoncé alionekana msanii mkubwa aliyekuwa akijaribu kitu kipya kwa kufanya kazi nayeye.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags