Saudia yaruhusiwa matumizi ya pombe
Wanadiplomasia kutoka nchini Saudi Arabia wamevunja marufuku ya uuzwaji wa pombe nchini humo baada ya kufungua duka la kwanza la vinywaji hivyo, maalumu kwa Wanadiplomasia wasio waisilamu jijini Riyadh.
Hii inakuja baada ya juhudi za Mwanamfalme Mohammed bin Salman kutaka kugeuza ufalme kuwa kivutio cha utalii na biashara.
Aidha tukio hilo limekuwa na maoni tofauti kwa wakazi wa Saudia kutokana na pombe kupigwa marufuku katika Uislamu.
Ikumbukwe kuwa mwaka 1952 Saudi Arabia ilipiga marufuku kuuzwa na kuingizwa kwa pombe katika nchi hiyo ambapo marufuku hiyo sasa imevunjwa baada ya miaka 72.
Leave a Reply