Saudi Arabia yatangaza kushiriki miss universe 2024 kwa mara ya kwanza

Saudi Arabia yatangaza kushiriki miss universe 2024 kwa mara ya kwanza

Kwa mara ya kwanza katika historia Saudi Arabia imeripotiwa kushiriki katika shindano la Miss Universe 2024, ikiwakilishwa na Miss Saudi Arabia 2021 Rumy Alqahtani (27).

Kupitia Ukurasa wa Instagram wa mwanamitindo Rumy Alqahtani alieleza furaha yake kwa kuwa mwanamke wa kwanza kutoka Saudia kushiriki mashindano hayo huku akiushukuru ufalme huo kwa kumchagua kuiwakilisha nchi hiyo.

Hii si mara ya kwanza wa Rumy Alqahtani kuiwakilisha nchi ya Saudia katika mashindano ya kimataifa ya urembo moja ya shindano alilowahi kushiriki ni la Februari mwaka huu la ‘Miss Global Asian nchini Malaysia’.

Rumy ana shahada ya kwanza ya Udaktari wa meno na ana uwezo wa kuongea lugha nyingi kwa ufasaha zikiwemo Kiingereza, Kifaransa, na Kiarabu.

Kutokana na maoni ya wadau mbalimbali wameeleza kuwa ushiriki wa Rumy Alqahtani katika shindano la Miss Universe 2024 ni hatua ya kihistoria kwa Saudi Arabia, ambayo inaashiria enzi mpya ya fursa kwa wanawake wa Saudi.

Shindano la Miss Universe, linatarajiwa kuanza Septemba 28, nchini Mexico, jukwaa ambalo linaadhimisha urembo, akili na utofauti wa kitamaduni.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags