WhatsApp imeweka feature mpya inayowaruhusu watumiaji wake kuweka wimbo wowote waupendao kwenye hadithi (status).
Kwa kutumia feature hiyo mpya unaweza kuchaguwa kipande cha wimbo cha sekunde 15 na kuweka katika status yako huku ikiambatana na picha
Jinsi ya kutumia feature hiyo
• Kwanza kabisa utaanza kwa ku-update WhatsApp kwenye Playstore au Appstore.
• Kisha fungua programu ya WhatsApp kwenye simu yako.
• Nenda kwenye sehemu ya kuweka hadithi (Status).
• Nenda kachague picha unayoipenda, utafuata process zilezile kama unataka kupost status
• Baada ya hapo kwenye simu yako juu utabonyeza sehemu ambayo ina muziki.
• Kisha chagua wimbo kutoka kwenye orodha ya nyimbo au pakua kipande cha wimbo unaotaka kuutumia, halafu chagua sekunde 15 na baada ya hapo unaweza kushare status yako.

Leave a Reply