Sara Akoko: Vijana tutumie muda tulionao kufanya vitu sahihi

Sara Akoko: Vijana tutumie muda tulionao kufanya vitu sahihi

Sara Akoko, ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anayechukua course ya Bachelor of Art in Geography and Environmental Studies.

Akoko anajihusisha na biashara ya kuuza vitu vya majumbani kama runinga, friji, majiko ya ovens yanayotumia gas na umeme, carpets, plastic flowers, mavazi ya watu wazima na watoto.

Ndani ya MwananchiScoop, Akoko anafunguka na kusema tatizo kubwa linalofanya watu wengi wasianzishe biashara au kuzikuza biashara zao si ukosefu wa mtaji bali ni ule uthubutu wa mtu mwenyewe.

Anasema mara nyingi mtaji umekuwa ukitumika kama sababu ya watu wasiumize vichwa ili kujua wanawezaje kuingia kwenye biashara.

“Sasa hivi kila mtu utakayeongea naye kuhusu biashara ataanza na tatizo la mtaji, ukimuuliza atautumiaje mtaji huo kama akiupata mara niyingi utakuta hana mpango maalumu unaoeleweka,” anasema

Anasema kwa upande wake yeye kabla ya kufikiria kufanya biashara alijiwekea malengo mazuri na alisema pndi atakapopata mtaji basi utamuwezesha kufika mbali zaidi.

“Mimi kama mnavyojua ni mwanafunzi na aliyenishawishi kufanya biashara ni dada yangu niliyemfuata kuzaliwa, basi nilikuwa nawwka akiba na kujipatia muda wa kufikisha kiwango cha mtaji niliyokuwa nataka na nilifanikiwa katika hilo na kuanzisha biashara yangu,” anasema

Anasema kama yupo kijana amemaliza chuo nab ado hajapata ajira namshauri afanye kazi yoyote anayoweza kufanya hata kama ina mshahara mdogo.

“Ikiwa lengo lako ni kukusanya mtaji, nategemea kazi hiyo utaifanya kwa bidii na kwa kipindi fulani kisha kuachana nayo na kuanzisha biashara ya ndoto yako,” anasema

Hata hivyo anasema wafanyabiashara na wale wanaohitaji kuanza kufanya biashara hawana budi kukubali kuteseka kwa muda kidogo ili waweze kufdika kule wanakotazamia.

Biashara yamsaidia kukidhi mahitaji

Akoko anasema biashara hiyo inamsaidia kukidhi mahitaji mbalimbali kipindi chote za chuo ikiwemo nauli (transport fees) ya kwenda na kurudi nyumbani pamoja na gharama za kujikimu chakula na vinywaji.

“Kiukweli ninashukuru hata hapa nilipofika, kupitia biashara ninayofanya sasa naweza kujikimu mahitaji yangu madogo madogo ya hapa na pale bila hata kuwasumbua wazazi wangu,” anasema

Changamoto

Anasema moja ya changamoto anayokumbana nayo ni pale mzigo wa biashara unapochelewa kufika, wateja uanza kulaumu na wakati mwingine kuhisi kama sio mwaminifu.

“Mimi ninanunua bidhaa China baada ya hapo ninazisafilisha hadi kufika Tanzania, sometimes mzigo unaweza kukaa hata miezi mitatu kwenye meli, hali inayosababisha kupoteza wateja wengi,

“Lakini pia wengine wanakuona kama sio mwaminifu na hiyo inatokana na kutokujua ni changamoto zipi tunapitia wakati wa kusubiria mzigo mpaka ufike hapa nchini,” anasema

Faida alizozipata

Anasema faida ni nyingi ila moja kubwa ni imemsaidia kujikimu mwenyewe hata baada ya kumaliza chuo bila kutegemea wazazi.

“Kipindi hiki ambacho nasubili kupata kazi ya ujuzi niliousomea nimeweza kujisaidia na kusaidia baadhi ya majukumu yanayoikabili familia yetu,” anasema

Ushauri wake kwa vijana

Akoko anasema ushauri kwa vijana wenzake ni kwamba, wautumie  muda walionao kwa kufanya vitu sahihi ambavyo baadae vitatusaidia kufikia malengo waliojiwekea.

Anasema pia watambue wanaweza kuanza biashara kidogo kidogo na baadae wakakuza bland hivyo wasisubiri mpaka wapate kiasi kikubwa cha fedha ndipo waanze.

“Ukisema usubiri mpaka upate kiasi kikubwa unachokifikiria itakuchukua muda mrefu sana na baadae utakata tamaa, anza kwa mtaji huo huo uliyonaop.

Aidha Akoko amefunguka na kusema kuwa anapenda kufanya modelling, na fashion design.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags