Sanjay Dutt kupewa ubalozi wa heshima Tanzania

Sanjay Dutt kupewa ubalozi wa heshima Tanzania

Serikali ya Tanzania inamuandaa msanii wa filamu kutoka nchini India, Sanjay Dutt kuwa balozi wa heshima kutokana na mapenzi yake kwa nchi na kuwa na wafuasi wengi watakaoona na kusikia kuhusu fursa za utalii nchini.

Mkurugenzi wa Utalii wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Thereza Mugobi ameyasema hayo jana Septemba 18, baada ya kumpokea msanii huyo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.

Amesema lengo la kumchagua Dutt ni kuingia kwenye soko la India yenye idadi ya zaidi ya watu 1.4 bilioni.

“Msanii huyu ni mkubwa nchini India, ukifuatilia mitandao yake ya kijamii ana wafuasi zaidi ya 200 milioni. Kwa hiyo akituma kuhusu Tanzania, fikiria kuhusu wafuasi wote hao na siyo Wahindi peke yake bali pia ni dunia nzima, hata mimi pia ni mfuasi wake. Hivyo tunaamini kwamba kituo cha Tanzania kitasikika katika soko la India na soko kubwa la Asia, ambako pia tunalenga kufikia huko,” amesema.

Maelezo hayo yameungwa mkono na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Damas Mfugale akisema kwa kumchagua msanii huyo watafanikiwa kupenya kwenye soko la utalii la India.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags