Sakata la Diddy laibuka tena

Sakata la Diddy laibuka tena

Baada ya ukimya wa miezi kadhaa sakata la mkali wa hip-hop kutoka nchini Marekani Sean Combs maarufu Diddy limeanza upya na sasa mawakili wake wamewasilisha ombi kufutwa kwa kesi inayodaiwa kuwa yeye na wenzake wawili walimbaka binti wa miaka 17 kwa kueleza kuwa madai hayo ni ya uongo.

Kwa mujibu wa tovuti AP imeeleza kuwa kesi hiyo iliyofunguliwa Desemba 2023 ikieleza kuwa Diddy na wenzake hao walimfanyia unyanyasaji wa kijinsia binti aitwaye Deo mwaka 2003 katika studio za kurekodia muziki New York.

Ukiachili na hilo mwanamuziki huyo pia aliwahi kukanusha madai yote ya kuhusishwa na unyanyasaji wa kijinsia yanayomkabili kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiweka wazi kuwa analifanyia kazi suala hilo na ukweli wote utajulikana.

Ikumbukwe kuwa Machi 25, 2024 makazi ya nyota wa muziki wa hip-hop, Sean "Diddy" Combs, ya Los Angeles na Miami yalifanyiwa upekuzi na Mawakala wa Usalama wa Taifa kama sehemu ya uchunguzi wa serikali kuhusu madai ya biashara ya ngono yanayomhusisha msanii huyo.

Diddy amekuwa akiandamwa na kesi za unyanyasaji wa kingono tangu mwaka jana 2023, kati ya waliowahi kumtuhumu ni aliyekuwa mpenzi wake Cassie.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags