Sadio Mane: Ninaimini tutashinda katika mchezo wa leo

Sadio Mane: Ninaimini tutashinda katika mchezo wa leo

Baada ya Sadio Mane kuondolewa katika michuano ya Kombe la dunia kwa mwaka 2022 kutokana na upasuaji wa mguu aliofanyiwa baada ya jeraha alilopata akiwa na Klabu yake ya Bayern Munich, nyota huyo wa Senegal ametumia ukurasa wake wa Instagram kuitakia timu yake ya Taifa ushindi inaposhuka dimbani Leo saa 1:00 usiku dhidi ya Netherlands.

Kupitia Instagram yake, Mane aliandika: “Wengi wenu mmenitumia ujumbe wa kutia moyo kufuatia jeraha langu. Namshukuru Mungu upasuaji ulikwenda vizuri. Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru nyote na kuonyesha shukrani zangu.

Leo nchi yetu pendwa inashiriki Kombe la Dunia Qatar 2022. Nina hakika kwamba watafanya vizuri na watauchukulia mchezo huo kama fainali halisi. Pia nina hakika kwamba Wasenegal wote watakuwa mbele ya runinga kuunga mkono na kuhimiza timu yetu shujaa ya Taifa,”

"Kama mashabiki wote wa Senegal, nina hakika kwamba wachezaji wenzangu watapambana kama mtu mmoja na kama kawaida ili kuwaheshimusha wapendwa wetu,” ameandika Sadio Mane.

Mane alijumuishwa katika kikosi cha Senegal kwa ajili ya michuano hiyo nchini Qatar licha ya ushiriki wake wa michuano hiyo kutiliwa shaka.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post