Sabaha: Watoto wangu wanatamani niache muziki

Sabaha: Watoto wangu wanatamani niache muziki

Msanii mkongwe wa muziki wa taarabu #SabahaSalum amedai kuwa watoto wake wanasauti nzuri ya kuimba lakini hawapo tayari na wanaomba Mungu aache kuimba taarabu.

Akizungumza na waandishi wa habari mkongwe huyo wa muziki wa mwambao ameeleza kuwa watoto wake wanaomba aache kufanya muziki, japo na wao wanasauti za kuimba ila hawako tayari kujihusisha na maswala ya muziki.

Haata hivyo msanii huyo ametoa wito kwa wanaotaka kufanya muziki wa taarabu kuwa wasiwe na wasiwasi muhimu ni kujitambua katika unachokifanya.

Msanii huyo ana takribani miaka 14 ndani ya muziki huo, amewahi kufanya nyimbo mbalimbali kama 'Niache nijivune', 'Hisani yangu', 'Tunapendana', 'Sihadhiriki', 'Aso mtu ana Mungu'.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags