Sababu ya Patoranking kuwa kimya kimuziki

Sababu ya Patoranking kuwa kimya kimuziki

Mwanamuziki kutoka Nigeria Patrick Nnaemeka 'Patoranking' amefichua kuwa ukimya wake kwenye muziki ulitokana na yeye kuwa masomoni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Patoranking ame-share picha zikifichua kuwa siku chache zilizopita alitunukiwa Shahada 'Degree' kutoka katika Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani akiwa ni mmoja wa wanafunzi waliohitimu darasa la BEMS 2024.

Patoranking alieleza kuwa yeye na wengine 35 wamepata Degree in Business, Entertainment, Media, and Sports (BEMS)’.

Mara ya mwisho Patoranking kuachia ngoma ni miezi saba aliyopita, aliachia video ya wimbo wake wa ‘Babylon’aliomshirikisha Victony ukiwa na zaidi ya watazamaji milioni 24.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags