Sababu ya kifo cha muigizaji Jacky ni upasuji kujiongezea urembo

Sababu ya kifo cha muigizaji Jacky ni upasuji kujiongezea urembo

Hatimaye uchunguzi wa maiti uliofanywa na wataalamu umethibitisha kuwa muigizaji na mfanyabiashara Jacky Smith aliyefariki dunia mwezi mei mwaka huu, alipoteza maisha kutokana na matatizo yatokanayo na upasuaji wa mwili kwa ajili ya urembo.

Nyota huyo alifariki katika Jimbo la Florida nchini Marekani baada ya kufanyiwa upasuaji uliolenga kumuongezea urembo.

Jacky ambaye alikuwa sehemu ya kipindi maarufu cha Wild N Out kinachoandaliwa na kuongozwa na Nick Canon, ameacha watoto wadogo watatu.

Hata hivyo tovuti ya jumuiya ya madaktari wapasuaji wa plastiki nchini Marekani imeweka wazi orodha ya hatari zinazohusiana na upasuaji wa aina hizo ambazo kati yake kuna kupoteza damu nyingi, kuganda kwa damu ndani ya mishipa au chemba za moyo, pamoja na matatizo ya moyo na mapafu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags