Leo tutaelezea kuhusu mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi wa mwanamke au ectopic pregnancy. Hili ni ni tatizo ambalo limetokea kuathiri wanawake mbalimbali.
MwananchiScoop imezungumza na Daktari wa Magonjwa ya binadamu kutoka Hospitali ya Anglikana, iliyopo Buguruni jijini Dar es Salaam, Dk. Rahel Mwinuka anafunguka na kusema Kwa kawaida, isipokuwa mara chache sana, mimba zitungazo nje ya mfuko wa uzazi hazina uwezo wa kukua kuwa mtoto kamili.
Dk. Mwinuka anasema mimba hizi ni hatari kwa afya ya mama mjamzito kwa vile humfanya kupoteza damu nyingi na hatimaye hata kusababisha kifo.
“Hata hivyo wasichana wanapaswa kutambua mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi inakuwa ni bahati mbaya, zile mbengu badala ya kwenda kuingia kwenye ile mirija ya Fallopian inatunga nje,
“Lakini tambua kuwa mimba ikitunga nje hakuna anayejua mpaka ndani ya miezi mitatu kwani lile yai kadiri litakavyokuwa linakuwa likimletea mtu maumivu makali na kutoka damu,” alisema
Alisema mtu anaweza asijigundua kama mimba yake ipo nje ya mfuko wa uzazi pale atakapopata maumvu makali ya tumbo licha ya kwamba anajiona ni mjamzito, hivyo akienda kupima lazima daktari ataona kuwa ipo nje ya mfuko wa uzazi.
Alisema mimba inayotunga nje ya mfuko wa uzazi mara baada ya kufika miezi miatu haiwezi kukua tena lazima itaharibika kwa kutoka yenyewe au kutolewa hospitali kwa mtu kufanyiwa oparesheni.
Aidha anafafanua kuwa kazi za mirija ya fallopian ni kusafirisha mayai kutoka katika kiwanda chake cha uzalishaji (ovary) mpaka kwenye mfuko wa uzazi (uterus).
Mwinuka alisema kuwa utungisho wa yai la kike na mbegu ya kiume hufanyika kwenye mirija hiyo ya fallopian.
“Mara baada ya utungisho, misuli inayozunguka mirija ya fallopian ikishirikiana na vinyweleo vilivyopo ndani ya mirija hii husukuma kiinitete au yai lililorutubishwa kulipeleka kwenye uterus.
“Yai lililorutubishwa, au kiinitete, lifikapo kwenye uterus hujipachika katika mojawapo ya kuta zake kwa ajili ya kuendelea kurutubishwa, kukua taratibu na hatimaye kufanya mtoto.
“Inapotokea misuli hii kushindwa kufanya kazi au vinyweleo hivi kukosekana, kiinitete hushindwa kusafirishwa kuingia kwenye uterus na hivyo hujitunga nje ya uterus na kusababisha ectopic pregnancy. Karibu asilimia 1-2 ya mayai yaliyorutubishwa hutunga nje ya mfuko wa uzazi wa mwanamke.Aidha, zaidi ya asilimia 95 ya mimba zinazotunga nje ya uterus hutokea kwenye mrija wa fallopian,” alisema.
Alisema mimba zinazotunga kwenye mrija wa fallopian husababisha kiinitete kujipachika katika kuta zake na hivyo kusababisha mishipa ya damu inayopita karibu na mrija wa fallopian kupasuka na damu kutoka kwa wingi hali ambayo isiposhughulikiwa mapema husababisha madhara zaidi na hata kifo.
AINA ZA ECTOPIC PREGNANCY
Alisema ni vema kuwajulisha kuwa kuna aina kuu nne za mimba zinazotunga nje ya mfuko wa uzazi, nazo ni, mimba zinazotunga kwenye mirija ya fallopian, mimba zinazotunga nje ya uterus na nje mirija ya fallopian, mimba zinazotunga ndani na nje ya uterus kwa wakati mmoja, mimba zinazojirudia kutunga nje ya mfuko wa uzazi.
Sababu za mimba kutunga nje ya mfuko za kizazi
Alisema sababu kubwa inayosababisha mimba kutunga kwenye mirija ya fallopian ni kushindwa kusafirishwa kwa kiinitete katika mirija hii hali inayotokana na mabadiliko katika hali ya mirija au uwezo duni wa mirija hiyo katika kusukuma kiinitete kuingia kwenye uterus kwa sababu ya ukosefu wa vinyweleo kutokana na magonjwa mbalimbali yanayoathiri muundo na maumbile ya mirija ya fallopian.
“Mimba zinazotunga kwenye mirija ya fallopian huwa zina madhara makubwa zaidi kwa sababu eneo hili ni jembamba mno kuweza kuhimili ukuaji wa mimba na pia lina mishipa mingi ya damu inayopita karibu ambayo ipo hatarini kupasuka hivyo kupelekea mgonjwa kupoteza damu nyingi sana.
“Mimba zinazotunga nje ya uterus na nje mirija ya fallopian: Baadhi ya mimba huweza kutunga kwenye kiwanda cha kuzalisha mayai (ovary), kwenye shingo ya uzazi (cervix) au ndani ya tumbo (intra-abdominal). Aina hii ya mimba ni chini ya asilimia tano ya mimba zote zinazotunga nje ya mfuko wa uzazi,” alisema.
Mwinuka alisema mmba inayotungwa ndani ya tumbo (intra-abdominal) wakati fulani huweza kutoa mtoto aliye hai tofauti na aina nyingine za mimba zinazotunga nje ya uterus. Hata hivyo uzalishaji wake hufanywa kwa operesheni ingawa hakuna ushahidi wa kitabibu kuhusu suala hili mpaka sasa.
“Madhara ya kutokea kwa upotezaji wa damu pamoja na maambukizi ni makubwa hivyo mara nyingi mimba za namna hii huhitaji kushughulikiwa haraka ili kumuepushia madhara makubwa mama mjamzito,” alisema.
Alisisitiza kuwa mimba zinazotunga ndani na nje ya uterus kwa wakati mmoja: “Wakati fulani, mayai mawili yaliyorutubishwa kwa wakati mmoja hutokea kupandikizwa sehemu mbili tofauti. Moja likipandikizwa nje ya uterus na jingine ndani ya uterus. Katika aina hii ya ectopic pregnancy, uwezekano wa yai lililotungwa ndani ya uterus kukua na kutoa mtoto ni mkubwa sana,” alisema
Leave a Reply