Sababu michezo ya wanawake kuvunjwa mwezi Disemba

Sababu michezo ya wanawake kuvunjwa mwezi Disemba

Ukiachana na ile kausha damu kumekuwa na michezo mingi yenye manufaa kwa wanawake ambayo hucheza kwa kuwekeza pesa zao, kukopeshana na kisha faida kugawana baadaye, utaratibu wa michezo hiyo mara nyingi huwa kila mwezi hutoa kiasi fulani cha pesa kutokana na hisa alizonunua mtu mwanzo.

Lakini uvunjwaji wa michezo mingi ya wanawake imekuwa ikivunjwa mwishoni mwa mwaka huku wanawake hao wakiwa wanakutana katika sehemu mbalimbali za sterehe kusherehekea pamoja kwa ajili ya tukio hilo, lenye lengo la kugawana mapoto ya mwaka mzima.

Kutokana na michezo hiyo kuwa mingi na kujizolea umaarufu kumekuwa na maswali mengi watu wakijiuliza, kwanini michezo hii huvunjwa mwishoni mwa mwaka. Fahamu kuwa wanawake huchagua mwezi Disemba kwa ajili ya kugawana fedha zote walizojiwekea kwa mwaka mzima, na fedha hizo huwa hazigawanywi pasu kwa pasu bali mwenye hisa nyingi ndiye huondoka na kitita cha kutosha.

Licha ya kugawana fedha hizo pia wanavikundi hawa huuchagua mwezi Disemba ili kuendana na mzunguko, malengo yao makubwa na kuanza upya michezo yao mwezi January katika mwaka mwingine.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post