Saba wakamatwa wakipanga shambulio la kigaidi

Saba wakamatwa wakipanga shambulio la kigaidi

Polisi kutoka nchini Ubelgiji, wamewakamata takribani watu saba siku ya alhamisi wanaoshukiwa kulisaidia kundi la Islamic State, na njama ya shambulizi la kigaidi kwa mujibu wa waendesha mashitaka.

Hata hivvyo haikuwekwa wazi ni wapi walikuwa wamepanga kufanya shambulizi hilo.

Lakini polisi wakisaidiwa na vikosi maalumu walivamia nyumba tisa katika miji kaadhaa magharibu mwa Ubelgiji katika operesheni iliyo ongozwa na jaji wa uchunguzi ambaye amebobea katika kesi za ugaidi.

Jaji huyo ataamua katika hatua za baadaye kama kuna ushahidi wa kutosha kuwafungulia mashitaka washukiwa hao kwa mujibu wa taarifa.

Aidha msemaji wa ofisi ya mwendesha mashitaka wa serekali kuu Eric Van Duyse, amekiambia moja ya chombo cha habari nchini humo kwamba walikuwa wakitaka kulenga taasisi iliyopo Ubelgiji, na wamekuwa wakitafuta silaha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags