Ruto ataka mapigano Sudan yasitishwe

Ruto ataka mapigano Sudan yasitishwe

Wajumbe wa kamati ya Mamlaka ya ushirikiano wa Serikali za Afrika Mashariki na pembe ya Afrika, (IGAD) ya kutafuta suluhisho kwa mzozo wa Sudan, wamekutana mjini Addis Ababa Jumatatu kujadili namna ya kusitisha mapigano na uhasama na kurudisha utulivu nchini humo.

Mkutano huo uliongozwa na Rais William Ruto wa Kenya kama mpatanishi wa IGAD na kujadili pia juu ya uwezo wa kupelekwa kikosi cha dharura cha kikanda ili kudumisha amani.

Mkutano huo ulifanyika mji mkuu wa Ethiopia, viongozi wa Kenya, na Ethiopia pamoja na mawaziri wa mambo ya nje wa Djibouti, Somalia na Uganda, pamoja na wajumbe wa Marekani, Umoja wa Mataifa, na wa serikali ya mpito ya kiraia nchini Sudan iliyopinduliwa na wanajeshi, wametaka pande zote mbili kusitisha mapigano na kuanza mazungumzo ya amani mara moja.

Aidha Rais Ruto amesema viongozi wa kijeshi wa pande zote mbili wanalazimika kusitisha mapigano bila ya masharti na kuanza mazungumzo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags