Rushayna atemwa ubarozi

Rushayna atemwa ubarozi

Hatimae aliyekuwa mke wa Haji Manara, Rushayna ametemwa ubalozi wa kutangaza nywele na Kampuni ya Uuzaji Nywele Bandia (Wigs), ikumbukwe kuwa Rushayna alipata ubalozi huo, mara baada ya ku-trend kwenye mitandao ya kijamii, kutokana na ndoa yake na Manara kuvunjika.

Emish ambae ni boss wa kampuni hiyo ya nywele, kupitia mahojiano na chombo cha habari alifunguka kumtema Rushayna, baada ya kuuliza kuhusiana na suala la balozi wa kampuni yake, Emish alifunguka na kusema kuwa,

 “kiukweli kwa sasa hivi tunamtafuta balozi mpya kwa sababu katika mabalozi waliopita tunaenda kwa mkataba na tunaangalia kafanya kazi gani na tumepata impact gani, wanakwambia ukitafuna bigii ikiisha utamu unaitema, kwa wakati ule alikuwa na utamu wake kwahiyo nitaangalia nani tena mwenye ladha ambaye nitampatia mkataba, Utamu wa rushayna umeisha”

“Sisi tunaangalia trend kwa ile aliyoipata niliangalia naweza kumtumia na biashara yangu ikaweza kwenda, mwisho wa siku akiisha utamu unamuweka pembeni maana yake huwezi ukatoa hela halafu usipate kitu, nikitoa million 5 natarajia kupata million 50, kwa wakati ule kupitia Rushayna nilipata nilicho kitaka ila siwezi kuendelea nae kwa sababu utamu wake umeisha sio tena kama mwanzo”.

Kutokana kauli hiyo ya Emish, Rushayna bado hajajibu chochote hadi sasa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags