Ruksa kusokota rasta shuleni

Ruksa kusokota rasta shuleni

Mahakama kuu nchini Malawi imeamuru mamlaka ya elimu kuwapokea wanafunzi waliosokota rasta katika shule za umma kote nchini.

Mahakama hiyo, iliyoko mashariki mwa jiji la Zomba, ilikuwa ikitoa uamuzi juu ya ombi lililowasilishwa na watoto wawili wa jamii ya Rastafari ambao walikataliwa kujiunga na shule za umma mwaka wa 2016 na 2010.

Wanafunzi hao wawili hata hivyo wamekuwa wakihudhuria shule baada ya kupata zuio la mahakama. Jaji Zione Ntaba alisema kuwazuia watoto wenye rasta kwenda shule ni kuwanyima haki yao ya kupata elimu.

"Wizara ya Elimu inapaswa kutoa tamko la kuruhusu watoto wote wa jamii ya Rastafari wenye rasta waruhusiwe darasani. Hili linapaswa kufanywa ifikapo tarehe 30 Juni," Jaji Ntaba amesema.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags