Ronaldo aweka rekodi mpya, afikisha mabao 900

Ronaldo aweka rekodi mpya, afikisha mabao 900

Staa wa soka dunia Cristiano Ronaldo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufikisha mabao 900.

Ronaldo amefikisha idadi hiyo ya mabao baada ya jana kuifungia timu yake ya taifa ya Ureno kwenye mchezo dhidi ya Croatia.

Katika mchezo huo wa Nations League Ureno imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Ronaldo alifunga bao hilo katika dakika ya 34 likiwa ni la pili kwenye mchezo huo, awali Diogo Dalot alitangulia kufunga katika dakika ya saba, lakini dakika ya 41 akajifunga na mechi hiyo kumalizika kwa ushindi upande wa Ureno.

Hivi karibuni staa huyo alisema anataka ahakikishe amefikisha mabao 1000 ndiyo ataachana na soka sasa akiwa amebakiza 100 tu akiwa na umri wa miaka 39.

Kwa mujibu wa mtandao wa transfermarkt, bao la kwanza la Ronaldo alifunga akiwa na Sporting Lisbon katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ureno dhidi ya Moreirense Oktoba 7, 2002.

Hata hivyo, wachambuzi wa soka awali hawakuwa wanaamini kama staa huyo leo angekuwa kwenye ubora huu unaozungumzwa kwenye dunia ya soka.

Ilimchukua Ronaldo miaka mitano kufikisha mabao 100, rekodi ambayo aliiweka kwenye mchezo dhidi ya Tottenham akiwa na Manchester United Januari 27, 2008 kwa bao la mkwaju wa penalti.

Wachezaji wenye mabao mengi

  1. Cristiano Ronaldo (Ureno) mabao- 900
  2. Lionel Messi (Argentina) mabao: 838
  3. Pele (Brazil): 762
  4. Romario (Brazil) mabao 755
  5. Ferenc Puskás (Hungary) mabao: 724






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post