Romy Jons kutoana jasho na Dj sinyorita, Dj ylb tuzo za mvaa

Romy Jons kutoana jasho na Dj sinyorita, Dj ylb tuzo za mvaa

Waandaji wa Tuzo za muziki za MVAA ambao wanajihusisha na utoaji wa tuzo katika vipengele mbalimbali kwa wasanii na vijana wachakarikaji Afrika wamemtaja kaka wa msanii wa Bongo Fleva Diamond, Romeo George, ‘Dj Romy Jons’, DJ YLB na DJ Sinyorita kuwania tuzo ya Dj bora wa club mwaka 2024.

MVAA wametoa orodha ya Ma-Dj 10 kutoka katika nchi mbalimbali akiwemo Dj Bookson (Congo), Dj Funkybee (Nigeria), na DJ Michel (Afrika Kusini) kupambania kipengele cha ‘Best Club Dj of the Year’.

Endapo official Dj wa Diamond, Romy atafanikiwa kuondoka na tuzo hiyo ataendelea kuwa katika kiwango kizuri na kutambulika zaidi, ikumbukwe mwaka 2022 alishinda tuzo ya ‘Dj Bora Wa Kiume Afrika Mashariki’ katika Tuzo za ‘EAEA 2022’ za Kenya.

Aidha licha ya kutajwa kuwania tuzo hizo Rj pia hivi karibuni ameweka wazi ujio wa ziara yake ya UDj aliyopa jina la ‘Rj The Dj Summertime Tour 2024’ atakayoifanya kwenye nchi tofauti tofauti katika club za usiku ikiwemo London, Toronto, United State huku usiku wa leo Julai 3, 2024 akitarajia kukiwasha katika club ya ‘Mantis’ iliyopo Dubai.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti yake rasmi ameeleza kuwa amewahi kunyakuwa Tuzo mbalimbali kubwa ndani na nje ya nchi kupitia uigizaji na Dj zikiwemo "DJ Bora" kwenye Tuzo za Muziki wa Bongo, Tuzo za AEA USA, Tuzo za EAEA, Tuzo ya Zikomo Awards na nyinginezo.

Pia kwa upande wa Mwanaisha Said maarufu DJ Sinyorita, aliwahi kushinda tuzo ya Afrima na kuipeperusha bendera ya Tanzania kwa kushinda Dj Bora Afrika tuzo zilizotolewa Desemba 21, 2021 nchini Nigeria.
.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post