Robinho ajifunza ufundi Tv gerezani

Robinho ajifunza ufundi Tv gerezani

‘Fowadi’ wa zamani wa Real Madrid, Manchester City na Brazil, Robinho ameanza kujifunza ufundi wa vifaaa vya umeme, ikiwamo kutengeneza televisheni akiwa gerezani huko kwao Brazil.

Staa huyo aliyewahi kuichezea pia ‘klabu’ ya AC Milan amehukumiwa kifungo cha miaka tisa jela baada ya kukutwa na hatia kwenye kosa la ubakaji na sasa ameamua kujifunza ufundi wa vifaa vya umeme akiwa huko gerezani.

Robinho, ambaye ni milionea baada ya kuripotiwa kuwa na utajiri wa Pauni 60 milioni, sasa anajifunza jinsi ya kukarabati televisheni mbovu, kutengeneza redio na vifaa vingine vya umeme ikiwa ni mradi maalumu wa kujifunza akiwa jela ili uje kumsaidia baadaye atakapotoka gerezani.

Mradi huo umelenga kuwafundisha wafungwa ujuzi mpya katika kujianda na maisha ya baadaye watakapotoka kifungoni.

Mwanasheria wa Robinho, Mario Rosso Vale, alisema mwanasoka huyo wa zamani amekuwa mfano mzuri huko gerazani tangu alipofungwa Machi.

“Robinho amekuwa mtulivu sana na amekuwa mfano mzuri kwa wafungwe wangine, hana matatizo kabisa. Na hata wamekuwa wakimpa viatu vya kuchezea soka, kwa sababu wakati mwingine wamekuwa wakicheza mechi,” alisema

“Katika kujishughulisha, ameamua kuingia kwenye mafundo ya ufundi wa vifaa vya umeme kama kutengeneza televisheni na radio mbovu. Amekuwa na saa 600 za kufanya kazi hiyo kwa ajili ya kujifunza na kuwa bora zaidi kwenye mpango huo.”
Robinho alikutwa na hatia baada ya kutajwa kwenye genge la watu waliofanya tukio la kumbaka mwanamke mmoja wa Kialbania kwenye kumbi moja ya starehe za usiku huko Milan, mwaka 2013.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags