Rihanna kurudi kwenye muziki kwa kishindo

Rihanna kurudi kwenye muziki kwa kishindo

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani, #Rihanna anadaiwa kuwa yupo kwenye mipango ya kurejea kwenye muziki kwa kishindo ambapo anatarajia kufanya ziara kubwa ya muziki mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo vinaeleza kuwa kurejea kwa mwanamuziki huyo ni kutokana na kusaini ‘dili’ nono lenye thamani ya ($32 million) ambazo ni zaidi ya Bilion 80 za kitanzania na ‘kampuni’ ya Live Nation.

Ujio huo unatajwa pia utasindikizwa na ‘album’ zake mbili ambazo ataziachia kuelekea ziara hiyo.

Ikumbukwe kuwa msanii huyo mwenye watoto wawili sasa, alipumzika kuimba kwa muda kwasababu zake binafsi, wimbo wake wa mwisho kutoa ni ‘lift me Up’ ambao mpaka sasa una miezi 11.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags