Miaka 28 ya kifo cha Notorious B.I.G

Miaka 28 ya kifo cha Notorious B.I.G

Siku kama ya leo Machi 9, 1997 ulimwengu ulimpoteza mkali wa muziki wa Hip-Hop Christopher Wallace ‘The Notorious B.I.G’ akiwa na umri wa miaka 24.

Kifo chake kilitokea baada ya kupigwa risasi nne huko Los Angeles, Marekani, alipokuwa amehudhuria kwenye sherehe za baada ya tuzo za Soul Training Awards usiku wa Machi 8, 1997.

Biggie alizaliwa Mei 21, 1972 huko Brooklyn New York nchini Marekani. Mama yake Volleta Wallace alikuwa mwalimu wa shule ya awali na Baba yake 'Selwyn George Latore' alikuwa Welder na Mwanasiasa. Wazazi wake wote walikuwa ni wakimbizi kutokea Jamaica.

Kutoka kwa albamu yake ya kwanza 'Ready To Die 1994' hadi 'Life After Death 1997' iliyotoka wiki mbili baada ya kifo chake, alifafanua vyema hadithi ya rap. Hata hivyo nyimbo zake kama “Juicy,’ ‘Big Poppa,’ ‘Hypnotize,’na ‘Sky's the Limit’ zinaendelea kuhamasisha vizazi vya wasanii na mashabiki mpaka sasa.

Licha ya kifo chake makubwa aliyofanya kwenye muziki, utamaduni na historia ya Hip Hop hayawezi kufutika kwani sauti yake bado inasikika katika mitaa ya Brooklyn na kwingine duniani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags