Rick Ross atangaza kuja Tanzania

Rick Ross Atangaza Kuja Tanzania

Star wa Hip Hop kutokea nchini Marekani Rick Ross ametangaza kuja Tanzania na kutembelea Mlima Kilimanjaro pamoja na mbuga ya wanyama ya Serengeti.

Hata hivyo msanii huyo amebainisha kuwa atakaa hapa nchini kwa muda wa siku saba na kuongeza kuwa amekuwa akiisikia mbuga na kuuona mlima huyo kwenye mitandao lakini sasa anataka kuuona mubashara.

“Nimekuwa nikipasikia Serengeti kwenye maisha yangu, lakini mimi mpaka kufika hapa leo kuna miaka 10 ya msoto nyuma, imefika muda sasa wa kufurahia maisha na uwezo ninao wa kwenda kutembelea Milima Kilimanjaro kwa muda wa wiki moja,” amesema

Hata hivyo staa huyo licha ya kujigamba kuwa na utitiri wa magari ya kifahari nyumbani kwake, hakuwahi kuruhusiwa kisheria kuendesha gari yoyote kutokana na kukosa leseni ya udereva.

Hivi sasa bosi huyo wa Maybach Music Group amepata leseni akiwa na umri wa miaka 45 baada ya kipindi cha karibu miongo mitatu kupita, ambapo ushawishi mkubwa amesema aliupata kutoka kwa Mama na dada yake ambao walikuwa wakimsumbua siku zote kwasababu wao ndio walikuwa wakimuendesha mara kadhaa.

Rozay amefunguka hayo kwenye mahojiano yake hivi karibuni wakati akikitangaza kitabu chake kinachoitwa "The Perfect Day to Boss Up".


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post