Rema aweka wazi kuwa na tatizo la macho

Rema aweka wazi kuwa na tatizo la macho


Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria, Rema ameweka wazi kuhusiana na uvaaji wake wa miwani kwa siku za hivi karibuni, ambapo ameeleza kuwa anatatizo la macho.

Rema ameyasema hayo wakati wa mahojiano yake na Capital Xtra katika usiku wa tuzo za Brit 2024 nchini Uingereza ambapo amebainisha kuwa amekuwa akivaa miwani mara kwa mara kutokana ana tatizo la kutokuona vitu vya karibu ambalo yupo nalo kwa muda mrefu.

Kwa Nigeria siyo Rema peke yake ambaye ameweka wazi kusumbuliwa na tatizo la macho, mwezi uliyoisha mwanadada Tiwa Savage aliweka wazi kuwa na tatizo la kutooni vizuri ‘uoni hafifu’ katika kusoma, vitabu na #Sms zinanazoingia katika simu yake, ndipo #Daktari wake akamshauri kutumia miwani muda wote, kutokana na hali kuwa mbaya zaidi katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags