Rayvany: Sasa hivi nafanya kazi na wasanii wa nyumbani tu

Rayvany: Sasa hivi nafanya kazi na wasanii wa nyumbani tu

Na Habiba Mohammed

Oyeeee!whats up whats up my beautiful people,Ebwana kwenye kona ya  entertainment kasimama mkali  katika game ya bongo fleva Chui maarufu Rayvany amesema kuwa anafanya kazi na wasanii wa nyumbani.

Rayvanny  alifanya mahojiano na kituo maarufu cha habari kwenye uzinduzi wa tamasha la muziki Fiesta huku  msanii huyo akitambulishwa  kutumbuiza kwenye tamasha hilo.

Katika mahojiano hayo Chui alisema”Namshukuru Mungu  na watayarishaji wa tamasha hili kunipa nafasi hii,mara ya mwisho kupanda kwenye jukwaa  hili kubwa la burudani mwaka 2016.”amesema Chui

Aidha msanii huyo alijibu swali ambalo limeulizwa sana kwenye kurasa za mitandao ya kijamii kuhusu kuto kuperform kwenye tamasha la Wasafi licha ya msanii kutoka kwenye label yake ya Nextlevel music  Macvoice kuperform kwenye tamasha hilo.

Rayvanny alifunguka na kusema kuwa  “Shows zinaendana na ratiba,huwezi kufanya show kwenye matamasha yote pia niliandika kwenye kurasa zangu za mitandao ya kijamii kwa sasa nafanya kazi na wasanii wa nyumbani”amesema msanii huyo.

Pia ameongeza na  kusema kuwa baadhi ya kazi alizofanya na wasanii wa nyumbani zimeshatoka na nyingine zipo kwenye maandalizi ya mwisho.
  
"baadhi ya kazi nilizofanya na wasanii wa nyumbani zimeshatoka na nyingine tupo kwenye maandalizi ya mwisho tuweze kuziachia mashabiki wakae tayari,kazi nzuri zinakuja” amesema Rayvanny

Shusha comment yako hapo chini .






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags