Rayvanny na Paula watoleana maneno

Rayvanny na Paula watoleana maneno

Waswahili bwana hawakukoseaga walivyosema mkiachana muachane kwa wema ili hapo baadae msije kutoleana maneno mabaya mkawafaidisha waja, basi bwana vita nzito ya kutupiana maneno inaendelea kupitia "Insta story' za mastaa wawili ambao ni Paula Masanja na Rayvanny ambao walikuwa wapenzi, vita hiyo imesababishwa na kitendo cha Rayvanny kuonekana kwenye tangazo la kipindi kipya cha "Behind the Gram" cha mwanadada Kajala na bintiye.

Ambapo Rayvanny na mke wake Faima wamewataka wenye kipindi hicho kufuta vipande ambavyo Rayvanny anaonekana, huku Paula akijibu kuwa Rayvanny alijipeleka mwenyewe kufanya kipindi hicho.

Wamekwenda mbali zaidi ambapo Rayvanny amedai alimuacha Paula baada ya kutembea na kaka yake kwenye muziki, huku Paula akisema kuwa anajutia kumjua Rayvanny maana alimtoa usichana wake na amesababisha dunia imuone yeye ni 'Malaya' jambo ambalo sio kweli.

Uwiiiiih! Vita bado ni mbichi kabisa, haya mwenetu sana fanya kukomenti hapo chini na utoe mtazamo wako katika hili je ilikuwa ni sawa kupelekana kwenye social media?.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post