Rayvanny kutumbuiza live MTV EMA 2021

Rayvanny kutumbuiza live MTV EMA 2021

Msanii wa muziki nchini Tanzania Rayvanny anakuwa msanii wa pekee kutoka Afrika ambaye amechaguliwa kupiuga show kwenye stage ya tuzo kubwa duniani za MTV EMA mwaka huu zinazotarajiwa kufanyika huko Hungary.

Kupitia official page za tuzo hizo wamethibitisha uwepo wa Rayvanny katika tuzo hizo ambapo atapiga shoo na imewekwa wazi kuwa nyimbo ya Mama tetema ambayo ameshirikiana na msanii Maluma itapigwa kwa mara ya kwanza kwenye tuzo hizo zitakaofanyika Arena kubwa ya michezo ya Laszio Papp Budapest iliyopo mji wa Budapest Hungary.

Hata hivyo hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rayvanny kwenda kupiga shoo katika mashindano lakini pia ni mara ya kwanza kwa wasanii wa Afrika Mashariki kupiga shoo na kupewa heshima na jina kuwa duniani katika muziki.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post