Kupitia ukurasa wa Instagram wa Vanny Boy ameshare picha ya mzazi mwenzie huyo huku akimuomba amsamehe kwa yote aliyowahi kumkosea.
“Kama nilikuchezea I’m sorry, this is my wife nampenda kuliko chochote kile, she’s my everything I love her so much @fahyvanny my life. Tamko Rasmi Naoa Mwezi Wa 5,”ameandika Chui.

Wawili hao wamekuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu tangu mwaka 2015 huku wakijaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Jayden.
Licha ya uhusiano wa wawili hao kuwavutia wengi katika mitandao ya kijamii lakini pia walihawahi kuachana mara kadhaa ambapo msanii Vanny Boy alianzisha uhusiano na mtoto wa mwigizaji wa zamani Kajala, Paula lakini mambo yakaenda kombo na kurudiana tena na mzazi mwenzie mwaka 2023.
Mbali na hayo Fahyma amewahi kuonekana kwenye video za nyimbo za Chui ikiwemo Natafuta Kiki (2016), Kwetu (2016), Mwambieni (2023), Forever (2023) na nyinginezo huku akiwa hajawahi kuonekana katika video za wasanii wengine zaidi ya Rayvanny.
Leave a Reply