Rayvanny azikwepa Tuzo za TMA

Rayvanny azikwepa Tuzo za TMA

Baada ya Kamati ya Uandaaji wa Tuzo za Muziki nchini (TMA) kutangaza baadhi ya vipengele na majina ya wasanii wanaowania tuzo hizo, mwanamuziki Rayvanny ametaka kuondolewa katika ushindani huo.

Vanny Boy amewaomba waandaaji wa tuzo hizo kumuondoa katika kipengele atakavyowania tuzo hizo huku akiwapisha wasanii wenzake waweze kumuwakilisha.

“Naheshimu jitihada za serikali yangu Wizara na Baraza kukuza Sanaa na muziki wetu wa Tanzania naunga mkono jitihada hizi kwa 100% ila sikubaliani na fitna za watu wachache, hivyo kwa unyenyekevu mkubwa naomba kutolewa katika tuzo zetu za TMA, kupisha wasanii wenzangu wataniwakilisha, am out,” ameandika Rayvanny

Hata hivyo hii siyo mara ya kwanza wa wasanii Bongo kuomba kuondolewa katika tuza hizo utakumbuka mwaka 2022 msanii wa muziki wa HipHop, Emmanuel Elibarick, maarufu Nay wa Mitego, alitangaza kujiondoa kwenye tuzo hizo huku sababu ikitajwa ni kukosa Imani na kamati ya uchunguzi wa kazi za muziki.

Mbali na huyo mwaka 2023 mwanamuziki Dully Sykes naye aliomba kuondolewa katika tuzo hizo huku sababu ya kuondolewa kwake haikufahamika.

Mbali na hayo ikumbukwe kuwa jana Agosti 29 Makamu Mwenyekiti wa TMA, Seven Mosha aliweka wazi kuwa wasanii wanaowania tuzo katika kipengele cha Mwanamuziki Bora wa Kiume wa Mwaka walichagua wenyewe nyimbo za kushindania.

“Kama mlivyoona hao ndiyo wasanii wetu bora wa mwaka jana napenda kukumbusha kwamba kitu ambacho tunajivunia na kufurahia katika tuzo za mwaka huu ni hao unaowaona wenyewe ndiyo waliingiza nominations zao kwenye vipengele tulivyotoa kwahiyo ni nyimbo ambazo wamechagua na walizozitaka wenyewe” alisema Seven






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags