Rayvanny ataka kuitwa Bill Gates

Rayvanny ataka kuitwa Bill Gates

Inavyoonekana trending ya wasanii wa Bongo kujiita majina ya wanyama huenda ikapotea baada ya baadhi yao kuelekeza nguvu zao kujiita majina ya matajiri au wafanyabiashara maarufu duniani.

Hii imekuja baada ya Harmonize kutaka kuitwa jina la mfanyabiashara na mmiliki wa Klabu ya Azam Said Salim Bakhresa, ambapo siku ya leo Rayvanny naye ametaka aitwa jina la Bill Gates tajiri na mfanyabiashara maarufu duniani.

Diamond Platnumz amewahi kujipa jina la Dangote tajiri namba moja barani Africa, Harmonize Bhakresa na Rayvanny Bill Gates.

Ikumbuke katika upande wa majina ya wanyama Diamond (Simba) Harmonize (Tembo) na Rayvanny (Chui) Young Lunya (Mbuzi) Shetta na Dudu Baya (Mamba) Country Wizzy (Fisi) Wema Sepetu (Twiga).






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags