Sean Atupwa Gerezani Baada Ya Kukosa Hela Ya Dhamana

Sean Atupwa Gerezani Baada Ya Kukosa Hela Ya Dhamana

Mwanamuziki wa Marekani, Sean Kingston ametupwa jela baada ya kushindwa kulipa dhamana ya dola 100,000 zaidi ya Sh 266 milioni, ambayo ingemfanya asiwekwe ndani wakati akisubiri hukumu yake.

Timu ya wanasheria wa mwanamuziki huyo Aprili 10, 2025 ilishindwa kutoa dhamana baada ya jaji wa kesi hiyo kuwaita mahakamani na kusikiliza shauri lao hilo la dhamana.

Utakumbuka, Sean Kingston na mama yake Janice Turner wanakabiliwa na madai ya kufanya udanganyifu wa biashara yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 1 za Kimarekani, ambapo kesi hiyo inahusisha vito vya thamani, magari ya kifahari, na bidhaa nyingine za gharama kubwa.

Waendesha mashtaka wanadai kuwa wawili hao baada ya kufanya udanganyifu kwa wafanyabiashara mbalimbali, kwa kutofanya malipo ya bidhaa hizo, bado waliendelea kutumia bidhaa hizo.

Mashtaka hayo ya udanganyifu wa mali zenye thamani ya zaidi dola milioni 1 yanahusisha udanganyifu kwa muuzaji wa magari baada ya kuchukua gari aina ya Cadillac Escalade yenye thamani ya dola 160,000. Pia kudanganya wauzaji wa vito vya thamani kwa bidhaa zenye thamani ya dola 480,000, na vitu vingine.

Katika kesi hiyo, hakimu aliamua mama wa Kingston abaki gerezani baada ya kuonekana yupo katika hatari ya kutoroka. Huku Kingston akipewa kufungo cha nje huku akisubiri hukumu yao Julai 11, 2025. Ambapo inaelezwa wanaweza kupata kifungo cha zaidi ya miaka 20 gerezani kwa kila shtaka moja kwa kila mmoja wao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags