Rapper Tyga akalia kuti kavu

Rapper Tyga akalia kuti kavu

Rapper kutokea nchini Marekani Tyga, unaweza kusema amekalia kuti kavu baada ya kufunguliwa mashtaka kwa kumpiga mpenzi wake wa zamani Camaryn Swanson maarufu kama Killa Cam usiku wa kuamka Jumatatu.

Taarifa zinaeleza kuwa Killa Cam alikuwa amelewa, lakini Tyga alimruhusu aingie ndani kwa ajili ya kuzungumza na baada ya muda zilisikika kelele za mpenzi wake huyo.

Mpenzi wake huyo ameiambia polisi kuwa T-Raww alikuwa akimshushia kipigo wakati wa majibizano yao ambapo leo atafika kituoni kutoa maelezo kwa upande wake ikiwa tayari amefunguliwa kesi ya unyanyasaji wa nyumbani.

Baada ya mambo hayo msanii Soulja Boy kupitia ukurasa wake wa Instagram alimchana makavu Tyga ambaye kwa sasa amejisalimisha kituo cha Polisi baada ya kustakiwa kwa kumpiga Ex wake.

Soulja Boy amesema Tyga anashida gani kwani amekalia tu kupiga wanawake na kungeza kuwa yeye ndio amerudi kwenye game kwa kishindo zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags