Rapa Malone amekanusha kutumia madawa

Rapa Malone amekanusha kutumia madawa

Mwanamuziki wa hiphop kutoka nchini Marekani Post Malone amekanusha kutumia madawa za kulevya baada ya maswali mengi  kuibuka kutokana na mabadiliko kwenye mtindo wake wa kufanya show na muonekano wake na kuwa karibu na binti yake.

Rapa huyo mwenye mtoto wa kike na mchumba wake, ambaye hajawahi kumuweka wazi kwenye mitandao ya kijamii au vyombo vya habari amefunguka na kueleza kuwa.

 "Situmii dawa za kulevya, nimeulizwa na watu wengi kuhusu kupungua uzito wangu na show zangu na enjoy sana kufanya show zangu na niko na afya njema zaidi, toka nimekuwa Baba nimeanza kuacha vitu kama Soda na nimeanza kula vizuri zaidi ili niwe karibu na mtoto wangu kwa muda mrefu zaidi” amesema Malone

Aidha alisisitiza kuwa maisha yake ya sasa anayafurahia na hakuna tatizo lolote kuhusiana na afya yake kwasasa kinachofuata kukaa studio muda mrefu ili kuendelea kutayarisha mziki wake  mpya.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags