Rambo kutoa kitabu kuhusu safari yake hadi kuwa staa

Rambo kutoa kitabu kuhusu safari yake hadi kuwa staa

Mwigizaji mkongwe kutoka Marekani Sylvester Stallone maarufu Rambo amefunguka kuja na kitabu chake kitachoelezea kuhusu safari yake hadi kuwa nyota mkubwa.

Kwa mujibu wa Tmz nyota huyo wa ‘Tulsa King’ ameweka wazi kuwa Riwaya yake itahusu safari yake kutoka kuwa mtu asiye na chochote hadi kuwa nyota wa filamu.

Mbali na hayo amedai kuwa ndani ya kitabu hicho ataeleza kwa undani safari ya kwenda New York wakati wa tamasha la Woodstock mwaka 1969 lilivyomkumbusha kuacha alama ulimwenguni.

Kitabu hicho kinatarajiwa kutoka mapema mwaka 2025 huku mwigizaji huyo akikazia kuwa kitasomwa kwa lazima hasa kwa mashabiki wa ‘Rambo’ na ‘Rocky’.

Sylvester Stallone ‘Rambo’ (78) amewahi kuonekana katika filamu mbalimbali zilizofuatiliwa ndani na nje ya nchi ikiwemo ‘Rambo’, ‘Rocky’, ‘The Expendables’, ‘Terminator’, ‘Creed’ na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags