Ramaphosa afuta huduma ya maji na umeme kwa Mawaziri

Ramaphosa afuta huduma ya maji na umeme kwa Mawaziri

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameondoa marupurupu yenye utata kwa mawaziri na manaibu wao ambao walikuwa zikisambaziwa umeme na maji bila malipo.

Manufaa hayo yalizua malalamiko kwa umma kwani yalionekana kutojali wakati raia wa Afrika Kusini wanakabiliwa na tatizo la kukatika kwa umeme kila siku na kupanda kwa gharama za maisha.

Katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu jioni, msemaji alisema rais "anakubali na kuthamini maoni ya umma juu ya suala hilo".

Haya watu wangu wa nguvu Nini maoni yako kuhusu mawaziri hawa kufutiwa huduma ya bure?

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags