Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amefuta sheria ya hukumu ya kifo na pia amebadili sheria ya ukosoaji wa Kiongozi wa Nchi kuwa kosa linaloadhibiwa kisheria.
Kupitia mabadiliko hayo Rais sasa amefuta sheria ya hukumu ya kifo na hivyo Watu hawatohukumiwa tena kunyongwa hadi kufa na pia kwa sasa Kiongozi wa Nchi anaweza kukosolewa bila anayemkosoa kukamatwa na kushtakiwa kuwa ametenda kosa la kisheria.
Msemaji wa Rais Hichelema, Anthony Bwalya amesema Rais Hichilema ameidhinisha kanuni ya adhabu ya mwaka 2022 inayofuta kutolewa kwa adhabu ya kifo na kosa la kumkashifu Rais, ambalo limekuwa kwenye vitabu vya sheria vya Zambia tangu enzi za kabla ya uhuru.
Wanaharakati wa haki nchini Zambia wamesifu hiyo hatua kubwa ya uamuzi wa kufuta sheria mbili za wakati wa ukoloni wa Uingereza ambazo haziendani na utawala wa kidemokrasia wa Taifa hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sera ya Mazungumzo Caroline Katotobwe amesema Raia wa Zambia sasa watakuwa na uhuru wa kueleza maoni bila kuogopa kufunguliwa mashtaka.
Leave a Reply