Rais wa Ukraine asema hatma ya mji wa Soledar

Rais wa Ukraine asema hatma ya mji wa Soledar

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema mapigano bado yanaendelea kwenye mji muhimu mashariki mwa nchi hiyo wa Soledar ambao mamluki wa kundi binafsi la ulinzi kutoka Urusi la Wagner walisema wameukamata.

 Kupitia ujumbe wa vidio anaoutoa kila siku kwa taifa, rais Zelensky amesema Urusi na washirika wake wanajaribu kufanya propaganda kwa madai ya kuukamata mji huo lakini ukweli ni kwamba mapambano bado yanaendelea.

Pande zote mbili yaan Urusi na Ukraine zimesema mapigano ya kuwania udhibiti wa mji huo ni makali na yamechukua muda mrefu huku Moscow ikitahadharisha madai ya ushindi wa mapema yanayotolewa na kundi la Wagner.

Mji wa Soledar wa kwenye mkoa wa Donetsk na unaofahamika kwa uzalishaji mkubwa wa chumvi, unapatikana kiasi maili tisa kutoka mji mwingine wa Bakhmut ambao vikosi vya Urusi vimekuwa vikijaribu pia kuukamata.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post