Rais Samia awasamehe wafungwa zaidi ya 300

Rais Samia awasamehe wafungwa zaidi ya 300

Rais wa Jmuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo April, 26 ametoa msamaha kwa wafungwa 376 ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano wa Tanzania, taarifa hiyo imetolewa leo na Waziri wa mambo ya ndani, Hamad Masauni.

Wafungwa sita kati ya walionufaika na msamaha huu wataachiliwa huru leo na wafungwa 370 watabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huo.

Msamaha huo ukiwa unaeleza kuwa “Ni mategemeo ya Serikali kwamba watarejea tena katika jamii kushirikiana na wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa letu na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags