Rais Samia atoa pongezi kwa Geay

Rais Samia atoa pongezi kwa Geay

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amempongeza mwanariadha kutoka Tanzania, Gabriel Gerald Geay kwa kushika nafasi ya pili kwenye mbio za Boston Marathon 2023 zilizofanyika Boston Massachusetts nchini Marekani.

Geay alitumia saa 2:06:04 kumaliza mbio zake huku aliyeshika nafasi ya kwanza Evans Chebet kutoka Kenya akitumia saa 2:05:54.



Kupitia ukurasa rasmi wa rais ameandika kuwa “Nakupongeza Gabriel Gerald Geay kwa kuwa mshindi wa pili katika Mashindano ya riadha ya Kimataifa ya Boston yaliyofanyika leo (jana) nchini Marekani. Jitihada zako zimeijengea heshima Tanzania. Nakutakia kheri katika kusonga mbele Zaidi, Serikali itaendelea kuwaunga mkono wanamichezo” ameandika Rais Samia






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags