Rais Samia atoa ndege kusafirisha kikosi cha Stars

Rais Samia atoa ndege kusafirisha kikosi cha Stars

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa ndege itakayotumika kuwasafirisha wachezaji wa ‘timu’ ya Taifa (Taifa Stars) kwenda Nchini Morocco ambapo watacheza na ‘timu’ ya Taifa ya #Niger katika kutafuta ‘tiketi’ ya kufuzu michuano ijayo ya Kombe la Dunia.

Taarifa  kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Gerson Msigwa imesema kuwa "Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan atoa ndege kwa ajili ya kuisafirisha Timu ya Taifa ya Soka kwenda Marrakesh Morocco ambako itaumana na Timu ya Taifa ya Niger katika kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ijayo ya Kombe la Dunia."

"Tunakushukuru sana Mheshimiwa Rais, sasa 'timu' itasafiri kwa muda mfupi kwenda Marrakesh tarehe 16 Novemba, 2023 na itarejea haraka tarehe 19 Novemba, 2023 baada ya mchezo wake wa tarehe 18 Novemba, 2023 dhidi ya Niger.”

“Kisha tarehe 21 Novemba itakuwa na kibarua kingine cha kuumana na Timu ya Taifa ya Morocco katika mbio hizohizo za kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia lijalo litakaloandaliwa na Marekani, Canada na Mexico."
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags