Rais mpya wa Brazil kuhudhuria hafla ya kumuaga nguli wa soka Pele

Rais mpya wa Brazil kuhudhuria hafla ya kumuaga nguli wa soka Pele

Saa chache baada ya kuapishwa kwake, Rais mpya wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva, anatarajiwa kuhudhuria hafla ya kumuaga nguli wa soka wa taifa hilo Pele.

Kiongozi huyo mpya alitaka kutoa heshima zake za mwisho kwa mshindi huyo wa Kombe la Dunia mara tatu kwa njia binafsi, na atasafiri leo Jumatatu hadi mji wa nyumbani wa Pele wa Santos ambapo hafla hiyo itafanyika.

Nguli huyo wa soka ambaye ni mchezaji pekee kuwahi kushinda Kombe la Dunia mara tatu mwaka 1958, 1962 na 1970, alifariki dunia siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 82 baada ya kuugua saratani ya utumbo.

Klabu yake ya zamani Santos imetangaza kuwa jeneza lake litaondoka hospitali ya Sao Paulo na litawekwa kwenye uwanja wa klabu hiyo ili umma wa Brazil upate fursa ya kutoa heshima zao za mwisho.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags