R.Kelly : Nina wasiwasi na maisha yangu humu gerezani

R.Kelly : Nina wasiwasi na maisha yangu humu gerezani

Mkali wa R&B kutoka nchini Marekani R.Kelly amwaga machozi, kwani kwenye sauti iliyodakwa na Rapa house tv akiweka wazi kwamba hapati huduma bora gerezani ikiwa ni baada ya kubainika ana tatizo la damu kuganda lililopelekea kuwa na hofu ya maisha yake gerezani.

kupitia sauti hiyo mwamba huyo amesikika akisema kwamba “Nina hofu na maisha yangu, kwani sipaswi kufa kwasababu ya chuki ya mtu ambaye hajali tatizo la mguu wangu” aliendelea kwa kueleza kuwa

“Vipi angekuwa baba yako, mama yako, mtoto wako au mtu umpendaye angepatwa na tatizo hili- (ungeshauri aende akapatiwe matibabu na daktari) lakini kwangu haikuwa hivyo, hata x-ray hamjanifanyia nina hofia maisha yangu katika eneo hili, ilikuwa karibu nife, kwani hata wanyama wanapewa huduma bora kuliko mimi” amesikika akisema R.Kelly

Ikumukwe tu Kelly kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa unyanyasaji wa kingono.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags