R.Kelly ahukumiwa miaka 20 jela

R.Kelly ahukumiwa miaka 20 jela

Mwanamuziki mkongwe kutoka Nchini Marekani R. Kelly amehukumiwa kifungo cha miaka 20 Jela huko Chicago kwa kesi yake ya uhalifu wa Kingono.

Waendesha mashtaka nchini humo walipendekeza Staa huyo afungwe kifungo cha miaka 25 na kuomba utolewe zaidi ya muda ambao tayari anatumikia jela.

Kelly alishtakiwa kwa kosa la kuwadhulumu watu 4, 3 wakiwa watoto wadogo, pia alikabiliwa na mashtaka ya ponografia ya watoto.

Alipatikana na hatia katika mashtaka 6 kati ya 13, huku mahakama ikimtia hatiani kwa makosa ya ponografia ya watoto.


Mashtaka dhidi ya mwamba huyo kutoka kwa Wakili wa Jimbo la Cook County , Kim Foxx yalitupiliwa mbali mnamo Januari, huku wakili wa mwanamuziki huyo Jennifer Bonjean  alisema Foxx  aliamua kutoendelea na kesi hiyo kwa sababu tayari amehukumiwa mara mbili kwa makosa sawa na tayari anaangalia uwezekano wa kufungwa maisha yake yote.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags