R. Kelly aishitaki serikali kwa kuvujisha taarifa zake

R. Kelly aishitaki serikali kwa kuvujisha taarifa zake

Nyota wa zamani wa R&B R.Kelly, ambaye anatumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono, ameishitaki serikali nchini Marekani kwa kosa la kuvujisha taarifa zake binafsi.

Wakili wa Kelly, Jennifer Bonjean aliwasilisha kesi hiyo jana Jumatatu katika mahakama ya shirikisho ya Chicago, ambapo inadai kuwa maafisa 60 wa Ofisi ya Magereza walitumia njia zisizofaa kurekodi matukio ya Kelly kati ya Julai 2019 hadi Januari 2020.

Ambapo inaelezwa kuwa baadhi ya maafisa magereza walimpatia taarifa binafsi za Kelly muandishi mmoja wa habari aliye fahamika kwa jina la Tasha K ambazo ni barua pepe, wageni wanao mtembelea na simu zake binafsi anazowapigia jamaa zake

R.Kelly kwa sasa anatumikia kifungoi chake cha miaka 30 katika gereza lililopo North Carolina.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post