R Kelly Miaka 30 Jela

R Kelly Miaka 30 Jela

Ebwana eeh moja kati ya taarifa ambayo imeendelea kuzua gumzo huko kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusiana na Mwanamuziki maarufu nchini Marekani Robert Sylvester Kelly   kuhukumiwa miaka 30 Jela.

R Kelly mwenye umri wa miaka (55) amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia katika mashtaka yaliyokuwa yakimkabili ikiwemo la unyanyasaji wa kingono kwa Wanawake na Watoto.

Hukumu ya R Kelly imetolewa katika mahakama ya shirikisho ya Brooklyn huko New York nchini Marekani.

Wanawake kadhaa walijitokeza mahakamani hapo kutoa Ushahidi wa namna R Kelly alivyowafanya watamani Kufa, ambapo Jaji Ann Donnelly, aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo alisema kuna Ushahidi mwingine wa waathiriwa ambao hawezi kuusahau kamwe.

Mawakili wa R Kelly wamemtetea mteja wao kwa kusema kwamba hapaswi kufungwa gerezani kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 kwa sababu alikuwa na maisha magumu akiwa mtoto, huku wakijaribu kuonesha kwamba wanawake wote waliomshtaki walikuwa na uhusiano nae wa kimapenzi na si kweli kwamba walifanyiwa vitendo hivyo bila ridhaa yao.

Mwanamuziki huyo ambaye ni Hodari wa utunzi wa nyimbo alifunguliwa mashtaka ya ulaghai na ulanguzi wa ngono mwaka jana katika kesi ambayo iliwakutanisha wasichana wengi Weusi waliowahi kufanyiwa vitendi hivyo na R Kelly

Aiseee tuambie mdau ni ngoma gani au mstari upi katika nyimbo zake unaukubali Zaidi? Dondosha comment yako hapo chini.

Comments 0

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.

Latest Post

Latest Tags