R Kelly Akutwa na Hatia

R Kelly Akutwa na Hatia

Mwanamuziki mkongwe nchini Marekani Robert Sylvester maarufuku kama R Kelly amekutwa na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 18, utekaji nyara, rushwa na biashara ya ngono.

Msanii huyo wa miondoko ya R&B pamoja na mambo mengine anadaiwa kutumia umaarufu wake na utajiri wake kuwarubuni wanawake kwa ahadi za kusaidia kazi zao za muziki.

Baadhi ya mashuhuda yaani waathirika wameiambia Mahakama kwamba walikuwa chini ya umri wa miaka 18 wakati wakinyanyaswa kijinsia na R Kelly.

Baada ya kukutwa na hatia hiyo hukumu yake inatarajiwa kutolewa Mei 4, 2022 na kuenda akahukumiwa kifungo cha miaka 10 au cha maisha gerezani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags